Bodi ya ligi kuu Tanzania (TPLB) imeufungia uwanja wa Ushirika uliopo jijini Moshi mkoani Kilimanjaro kuchezewa mechi zozote za mashindano kutokana na kukosa baadhi ya sifa za kikanuni kama zilivyoainishwa kwenye kanui ya sasa inayozungumzia uwanja na sheria namba moja ya mpira wa miguu unaozungumzia uwanja.
Kutokana na uamuzi huo wa kuufungia uwanja wa Ushirika,Bodi ya ligi imeitaka klabu ya Polisi Tanzania kuutumia uwanja wa Sheikh Amri Abeid uliopo jijini Arusha kwa ajili ya mechi zake za nyumbani za ligi kuu ya vodacom 2020/2021.
Kamati ya leseni ya klabu itaufanyia ukaguzi uwanja huo baada ya marekebisho kukamilika.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.