Bodi ya ligi kuu nchini (Tplb) imebariki uamuzi wa klabu ya Yanga sc kumtumia uwanja wa Kmc Complex uliopo Mwenge jijini Dar es Salaam kama uwanja wa nyumbani katika michezo yake iliyosalia ya ligi kuu ya Nbc nchini.
Awali klabu hiyo ilikua inautumia uwanja wa Azam Complex Chamazi jijini Dar es Salaam lakini baada ya kupoteza michezo miwili dhidi ya Klabu za Azam Fc na Tabora United moja kwa moja klabu hiyo itangaza kuhama uwanja na kuandika barua ya kuomba ridhaa kwa bodi hiyo yenye mamlaka ya kusimamia ligi kuu nchini.
Taarifa kwa Umma iliyotolewa na bodi hiyo imeonyesha kukubali ombi la klabu hiyo kupitia kanuni ya 9:4 ya ligi kuu kuhusu uwanja.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Yanga sc baada ya kukubaliwa ombi hilo sasa itaungana na klabu za Simba sc,Kmc Fc,Simba queens na Yanga Princess kama timu zitakazo kuwa zinatumia uwanja huo kama uwanja wa nyumbani.