Home Makala “Tukutane Msimu Ujao” Ahmed Ally

“Tukutane Msimu Ujao” Ahmed Ally

by Sports Leo
0 comments

Msemaji wa klabu ya Simba sc Ahmed Ally amesema kwamba kama klabu msimu huu hawana cha kujivunia huku akisisitiza kuwa wanajipanga kwa msimu ujao wa ligi kuu na michuano ya kimataifa.

Ahmed alisema hayo dakika chache baada ya kutamatika kwa msimu huu ambapo tuzo za washindi binafsi za ligi kuu na michuano ya kombe la shirikisho zikitolewa mkoani Tanga huku Mh.Hamis Mwinjuma ambaye ni Naibu waziri wa Utamaduni,Sanaa na michezo akihudhuria kama mgeni Rasmi.

“Kwetu Simba tuwapongeze nyota wetu waliotwaa tuzo hakika wametuheshimisha. Kiujumla kama timu hatuna cha kujivunia sana maana hatujapata tulichokihitaji msimu huu,” Aliandika Ahmed kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram.

banner

Msemaji huyo machachari aliongeza kuwa “Hii inatupa nafasi ya kujipanga zaidi kwa msimu ujao. Ubingwa unahitaji wachezaji bora na timu imara. Ni jukumu letu viongozi kutafuta wachezaji sahihi na kutengeneza timu madhubuti, na hilo limeshaanza kufanyika kwa umaridadi wa hali ya juu sana,”.

“Timu kubwa kama Simba haipaswi kukaa muda mrefu bila mataji, miaka miwili inatosha ni muda sasa wa kurudisha ufalme na wetu. Tukutane 2023/2024,”Alimalizia kusema.

Katika usiku huo wa tuzo mchezaji wa klabu ya Simba sc alizoa tuzo za kiungo bora wa ligi kuu ya Nbc,Mchezaji muungwana na tuzo ya mfungaji bora waliyogawana na Fiston Mayele huku kwa upande wa klabu ya Simba sc wakiwa wamemaliza msimu huu bila kupata tuzo yeyote.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited