Home Makala “Tunawaheshimu” Kocha Simba sc

“Tunawaheshimu” Kocha Simba sc

by Sports Leo
0 comments

Kocha wa Simba sc Roberto Oliveira “Robertinho” amesema kuwa wao kama klabu wanaiheshimu sana timu ya Raja Casablanca ambao watakutana nao hapo kesho katika mchezo wa hatua ya makundi ya klabu bingwa barani Afrika utakaofanyika katika uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es salaam.

Kocha huyo raia wa Brazil alizungumza hayo mapema hivi leo wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika mapema hivi leo jijini Dar es salaam.

“Kila mechi kwenye michuano hii ni ngumu, tunaiheshimu Raja Club Athletic 🇲🇦, ni timu nzuri na inahistoria kubwa katika soka la Afrika lakini malengo yetu ni kuhakikisha tunashinda nyumbani” Alisema kocha huyo wa zamani wa Vipers Fc ya nchini Uganda.

banner

“Simba ni timu kubwa, ina malengo ya kufika mbali na ikiwezekana hata kuchukua UBINGWA wa Africa lakini ili iwezekane inapaswa kuanzia kwenye hatua hii”

Simba sc inapaswa kushinda mchezo huo tayari kuanza kukusanya alama za kuitafuta robo fainali ambapo washindi wawili wa kila kundi watafuzu hatua hiyo huku Simba sc wakiwa katika kundi C na Horoya Fc,Raja Casablanca na Vipers Fc.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited