Home Makala Usajili wa Neymar Balaa Tupu

Usajili wa Neymar Balaa Tupu

by Sports Leo
0 comments

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Brazil Neymar Dos Santos amekamilisha usajili wa kujiunga na klabu ya Al Hilal Fc ya nchini Saud Arabia kwa dau la paundi milioni 86 akitokea katika klabu ya Paris St.German ya nchini Ufaransa.

Neymar amesaini mkataba wa miaka miwili na klabu hiyo huku akilipwa pesa kufuru kiasi cha paundi milioni 2.5 kwa wiki kama mshahara wake ambapo kwa mwezi atapokea jumla ya kiasi cha paundi milioni 10.

Psg imelazimika kumuuza mchezaji huyo ili kukabiliana na sheria za matumizi ya fedha ya shirikisho la mpira wa miguu duniani (Fifa) ambapo msimu uliopita walipigwa faini ya paundi milioni 56 kwa kukiuka sheria hiyo hivyo kupokea kiasi cha paundi milioni 86 kwa kumuuza Neymar imekua nafuu kwao kwa maana ya kupunguza pia kiasi cha mishahara ambapo kwa msimu alikua analipwa takribani paundi milioni 25.

banner

Kocha Luis Enrique haonekani kumuhitaji sana staa huyo na hata alidiriki kumuacha nje ya kikosi katika mchezo dhidi ya Fc Lorient uliomalizika kwa suluhu.

Neymar tangu ajiunge na Psg amefunga magoli 118 huku tofauti na walivyofikiria matajiri wa klabu hiyo alishindwa kuisaidia klabu hiyo kunyakua taji la klabu bingwa barani ulaya.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited