Mitambo maalumu ya kumsaidia refa kutoa maamuzi sahihi katika michezo maarufu kama Var (Video Assistant Reffaree) tayari imeshafungwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam ambapo utafanyika mchezo kati ya Simba sc dhidi ya Orlando Pirates wa hatua ya robo fainali ya kwanza ya kombe la shirikisho.
Var inatarajiwa kufanyiwa majaribio leo saa moja usiku ambapo kutakua na mazoezi ya timu ya Orlando Pirates ambapo wamewasili usiku ya kuamkia leo wakitokea Nairobi Kenya.
Kwa mujibu wa taratibu za mitambo hiyo itafanyiwa majaribio kwa saa nne mfululizo kuona kama inafanya kazi kwa usahihi ili kuweza kuhimili kuchukua matukio yote ya mchezo huo siku husika.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Hii ni mara ya kwanza kwa mitambo hiyo kutumika nchini tangu igunduliwe huku pia ikiwa ni mara ya kwanza kwa uwanja wa Benjamin Mkapa kufungwa mitambo hiyo.