Miamba ya soka ndani ya Ligi Kuu England ikiwa ni pamoja na Liverpool, Manchester United na Arsenal imegongana kwenye kuwania saini ya winga anayekipiga ndani ya klabu ya Monaco, Wissam Ben Yedder.
Nyota huyo mwenye miaka 29 alijiunga na AS Monaco akitokea klabu ya Sevilla na amekuwa nyota ndani ya Ligue msimu huu ambapo ametupia mabao 18 akiwa amecheza mechi 26 hii imemfanya kuwavutia klabu nyingi kubwa ambazo zinahitaji kuipata saini yake kwa ajili ya kumtumia msimu ujao wa 2020/21.
Mbali na timu ambazo zinashiriki Ligi Kuu England,pia timu zinazoshiriki La Liga zinahaha kuipata saini ya nyota huyo huku Real Madrid ikitajwa kuwa mstari wa mbele.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.