Klabu ya Yanga sc wapo katika hatua nzuri za mazungumzo ya kumsajili winga raia wa Ivory Coast Aubin Kramo Kouame ambaye kwa sasa anakipiga katika klabu ya Asec Mimosas inayoshiriki ligi kuu nchini humo,
Kramo mwenye umri wa miaka 27 anatumia zaidi mguu wa kushoto huku akiwa anamudu vyema kucheza winga zote za kulia na kushoto ambapo msimu uliopita alifanikiwa kuifungia timu hiyo mabao tisa na kutoa pasi nane za mabao.
Chanzo kutoka nchini Ivory Coast kimeeleza kuwa Yanga s wapo katika mazungumzo ya kumsajili winga huyo ambaye ni moja kati ya wachezaji bora ndani ya Ligi kuu ya Ivory Coast ili kuziba nafasi ya Tuisila Kisinda ambaye amerudi katika klabu yake ya Rs Berkane baada ya mkataba wake wa mkopo kuisha.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Yanga sc inamsajili winga huyo ili kuboresha mashambulizi kutokea pembeni ikiwa tayari imembakisha Jesus Moloko huku sasa ikitafuta winga kuja kuziba pia nafasi ya Benard Morrison ambaye ina mpango wa kuachana nae.