Nyota wa zamani wa timu ya Barcelona, Xavi Hernandez amefunguka kuwa kwa sasa ni wakati sahihi kwa yeye kurejea na kuinoa klabu yake ya zamani.
Xavi baada ya kustaafu kama mchezaji kwa sasa ni kocha ambaye anakinoa kikosi cha Al Sadd nchini Qatar na anafurahia maisha huko japo kwa sasa anatamani kuona siku moja anarejea katika klabu yake ya Barcelona na kwenda kuifundisha hii ni baada ya kuwa vizuri.
“Nimeshajipima mwenyewe kama kocha tayari kwamba sasa naweza kupambana na ndoto yangu ya kwenda kuifundisha Barcelona naona huenda ikatimia siku moja kutokana na hili ambalo naliamini mimi”alisema Xavi