Yanga Sc imekamilisha usajili wa wachezaji wawili kwa mpigo kutokea nchini DR Congo kwenye klabu ya As Vita ambao ni Mukoko Tunombe na Tuisila Kisinda.
Wote wawili wamekubali kumwaga wino wa kuitumikia klabu hiyo kwa miaka miwili jana usiku na kutinga rasmi uzi wa Jangwani kuashiria ni miongoni mwao tayari kwa msimu wa 2020/2021.
Mkurugenzi wa uwekezaji wa GSM,Hersi Said ambaye pia anahusika zaidi kusimamia usajili wa wachezaji Yanga Sc ametumia takribani siku mbili kuwachukua wachezaji hao lakini bado kuna kifaa kingine wanakihitaji kutoka As Vita ambaye atahusika zaidi kufunga mabao.