Home Makala Yanga sc Balaa Tupu

Yanga sc Balaa Tupu

by Sports Leo
0 comments

Ndivyo unavyoweza kusema kwa sasa kutokana na timu hiyo kuwa na mfululizo wa matokeo mazuri ya ushindi wa mabao mengi hasa katika michezo yake miwili ya mwisho ambapo wamefanikiwa kuifunga Kmc 5-0 na Asas Fc 5-1 na kufanikiwa kufuzu hatua inayofuatia ya michuano yaklabu bingwa barani Afrika.

Yanga sc katika mchezo huo wa mwisho wa kuwania kufuzu hatua ya pili ilipata mabao hayo matano kupitia kwa Max Nzengeli,Hafiz Konkoni,Clement Mzize na Pacoma Zouzou na kufuzu kwa ushindi wa jumla wa mabao 7-1.

Mbali na kupata ushindi huo Yanga sc imefanikiwa kucheza soka la kiwango cha juu huku pia kocha Miguel Gamondi akifanikiwa kuwapa muda wa mapumziko baadhi ya mastaa wake kama Khalid Aucho,Mudathir Yahaya,Dickson Job,Yao Kouasi na wengineo huku akiwarejesha kipa Djigui Diara na nahodha Bakari Mwamnyeto ambao walikosekana katika mchezo dhidi ya Kmc.

banner

Yanga sc sasa ina kibarua kigumu katika hatua hiyo ya pili ambapo watakutana na El-Merreckh Fc ya nchini Sudan ambao kwa sasa wanatumia viwanja vya nchini Rwanda kama nyumbani baada ya nchi yao kukutwa na machafuko huku pia ikidaiwa wana mpango wa kupeleka mchezo huo wa kwanza nchini Morroco.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited