Klabu ya Yanga sc imezidi kuonyesha ubabe dhidi ya timu nyingine za ligi kuu baada ya kuifunga klabu ya Ruvu Shooting kwa mabao 2-0 katika mchezo hatari wa ligi kuu uliofganyika katika uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es salaam.
Katika mchezo huo Yanga sc ililazimika kusubiri mpaka kipindi cha pili ili kupata bao la uongozi kupitia kwa Feisal Salum dakika ya 52 akifunga kwa kichwa krosi safi ya Joyce Lomalisa Mtambala kutokea upande wa kushoto wa uwanja bao ambalo lilirudisha morali kwa mashabiki wa klabu ya Yanga sc hali iliyopelekea kushangilia kwa nguvu na hatimaye kufanikiwa kupata bao la pili dakika ya 71 ya mchezo kupitia kwa Bakari Mwamnyeto.
Yanga sc kutokana na ushindi huo sasa imefikisha alama 13 ikiwa juu kileleni mwa msimamo wa ligi kuu nchini ikitanguliwa na Simba sc kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa huku wiki hii ikiwa na mchezo mgumu wa kimataifa dhidi ya Al Hilal siku ya jumamosi.