Home Makala Yanga sc Kamili Gado

Yanga sc Kamili Gado

by Dennis Msotwa
0 comments

Ikiwa inaongoza katika msimamo wa ligi kuu nchini klabu ya Yanga sc imeendelea na maandalizi kuelekea mchezo dhidi ya klabu ya Kmc utakaofanyika machi 19 katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Kocha wa klabu hiyo mwenye uraia wa Tunisia Nasreddine Nabi tayari anafurahia urejeo wa mastaa wake Saido Ntibanzokiza,Khalid Aucho na Farid Musa huku winga Chico Ushindi akiwa njiani kupona marelia yanayomsumbua na kumfanya akose mchezo uliopita dhidi ya Geita Gold Fc uliofanyika katika uwanja wa Ccm Kirumba ambapo Yanga sc waliibuka na ushindi wa 1-0.

Kuhusu mchezo kocha Nabi alisema“Kila mtu anajua uwezo wa KMC, hii ni miongoni mwa timu bora kwenye ligi kuu na ni wazi tunatarajia mchezo mgumu dhidi yao, hasa kutokana na ukweli kuwa sehemu kubwa ya kikosi chao kina wachezaji wazoefu.

banner

“Lakini licha ya ushindani tunaotarajia kukumbana nao ni lazima tuhakikishe tunashinda mchezo huu, nilazima mawazo yetu yawe juu ya pointi tatu na si matokeo ya aina nyingine na wachezaji wangu wanajua hilo.”Alimalizia kocha huyo anayesifika kwa kupenda nidhamu ya hali ya juu.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited