Klabu ya Yanga sc imefikia makubaliano ya kuachana na mshambuliaji Kennedy Musonda ambaye mkataba wake unaelekea ukingoni msimu huu.
Staa huyo aliyesajiliwa miaka mitatu iliyopita kutokea klabu ya Power Dynamos ya nchini kwao Zambia ambapo ilitarajiwa angekua mbadala wa mshambuliaji Fiston Mayele aliyeondoka klabuni hapo msimu mmoja uliopita na kujiunga na Pyramid Fc.
Hata hivyo Musonda ameshindwa kuwa na uhakika wa nafasi pamoja na Mayele kuondoka klabuni hapo ambapo amekua akianza mara chache na muda mwingine akikosa nafasi kabisa.
Mabosi wa Yanga sc pamoja na kumleta Prince Dube msimu huu pia wanaona ni vyema kuongeza nguvu eneo la ushambuliaji ambapo wanamtolea macho Jonathan Sowah wa Singida Black Stars.
Tayari mshambuliaji huyo ameshapewa taarifa kuhusu kutoongezewa mkataba na mabosi wa klabu hiyo na ndio sababu ya kufuta picha nyingi akiwa na klabu hiyo katika mtandao wake wa Instagram.
Sasa Musonda anaangalia ofa alizonazo ili aamue atajiunga na klabu gani msimu ujao.