Home Makala Yanga sc Kuwakabili Al Hilal

Yanga sc Kuwakabili Al Hilal

by Sports Leo
0 comments

Baada ya kuiondosha klabu ya Zalan Fc kwa idadi ya mabao 9-0 katika michezo miwili klabu ya Yanga sc sasa itakutana na klabu ya Al Hilal Omdurman ya nchini Sudan katika hatua ya pili ya michuano ya kombe la klabu bingwa barani Afrika ambapo Yanga sc itaanzia nyumbani nchini Tanzania.

Yanga sc itakutana na Al Hilal inayonolewa na kocha Frolent Ibenge baada ya kuifunga Zalan Fc katika ujumla wa mabao 9 katika michezo miwili ambayo yote ilifanyika nchini Tanzania katika uwanja wa Benjamin Mkapa na Al Hilal ikiwatoa St.George ya nchini Ethiopia kwa jumla ya mabao 2-2 ambapo Wasudani hao wamepita kwa bao la ugenini baada ya mchezo wa pili nyumbani kushinda 1-0 huku mchezo wa awali ugenini wakifungwa 2-1.

Yanga sc inafaida ya kocha wake mkuu Nasreddine Nabi kufundisha soka nchini Sudan akiifundisha Al Hilal na El Merreckh zote za nchini humo huku pia akiwa na hasara ya kocha Ibenge kuwafahamu zaidi wachezaji mastaa wa klabu ya Yanga sc kwa kuwa amewafundisha katika klabu ya As Vita ambapo wengi amewalea wakiwemo kina Djuma Shabani,Fiston Mayele,Jesus Moloko,Tusila Kisinda na Yannick Bangala ambao ni panga pangua katika kikosi cha kwanza cha Yanga sc.

banner

Michezo hiyo inatarajiwa kufanyika kati ya tarehe 7 oktoba na 14 oktoba ambapo Yanga sc itaanzia nyumbani kisha itasafiri kwenda ugenini kucheza katika uwanja wenye fujo nyingi za mashabiki wa klabu hiyo ya Al Hilal omdurman.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited