Klabu ya Yanga Sc kesho wanatarajiwa kuingia dimbani kuwania alama tatu muhimu katika mchezo wa Ligi Kuu ya Nbc dhidi ya klab ya Namungo Fc mchezo utakaofanyika katika uwanja wa Kmc Complex Jijini Dar es Salaam.
Kwasasa Yanga sc inaongoza msimamo wa ligi kwa alama 70 na siku ya kesho Mei 13 itavaana na Namungo FC inayoshika nafasi ya 9 ikiwa na pointi 31 katika mchezo huo unaotarajiwa kuwa mkali.
Kwa mujibu wa Takwimu katika michezo mitano ya mwisho baina ya timu hizi mbili Yanga sc imetawala kwa ushindi mfululizo katika michezo hiyo ikifunga magoli 9 na kufungwa 2.
“Tusisahau lengo letu namba moja ni kuchukua alama tatu ili tubakie kileleni, najua pia Namungo Fc wanahitaji alama moja tu ili wasalie ligi kuu, sisi tunapaswa kufanya kila kitu tusifanye makosa ili tusipoteze utofauti wa alama moja uliopo kwa Simba SC”,Alisema kocha Miloud Hamdi wa klabu ya Yanga Sc wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Yanga sc ikishinda mchezo wa kesho itafikisha alama 73 na kuzidi kutanua pengo la alama baina yake na Simba sc.