Home Makala Yanga sc Vs Mazembe Caf

Yanga sc Vs Mazembe Caf

by Dennis Msotwa
0 comments

Shirikisho la soka barani Africa (Caf) limefanya droo wa makundi ya kombe la shirikisho ambapo klabu ya Yanga sc imeangukia katika kundi D lenye timu za Tp Mazembe ya Congo,Us Monastry ya Tunisia na Real Bamako ya nchini Mali katika michuano ambayo inatarajiwa kuanza mwezi Februari 2023.

Katika Droo hiyo wasiwasi wa Watanzania wengi ulikua ni kupangwa kundi moja na timu za Uarabuni ambazo zimekua vizuri kiuchumu hivyo kusumbua barani Afrika zikiwemo kutwaa ubingwa wa mashindano mengi ya Caf kwa ngazi za klabu.

Yanga sc itaanzia ugenini katika mchezo wa kwanza Februari 12 ikisafiri nchini Tunisia kuwavaa Us Monastriene kisha itarejea nchini kuvaana naTp Mazembe Februari 19 na baadae Februari 26 itasafiri mpaka mji mkuu wa Mali wa Bamako kuvaa na Real Bamako Februari 26 na kisha March 8 itaruduana na Real Bamako nchini.

banner

March 16 Yanga sc itawakaribisha Us Monastriene hapa nchini na kisha itakwenda Congo kumalizana na Tp Mazembe April 2 na kama itakua imejinyakulia alama za kutosha basi itafuzu hatua ya robo fainali ya michuano hiyo ya pili kwa ukubwa kwa ngazi za klabu barani Afrika.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited