Mchezo wa fainali ya kombe la shirikisho barani Africa utawajumuisha Yanga sc dhidi ya Usm Algers ya nchini Algeria ambapo timu hizo zimefanikiwa kufuzu katika hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo ya pili kwa ukubwa kwa ngazi za vilabu barani Afrika.
Yanga sc imefanikiwa kuwaondosha Marumo Gallants ya Afrika ya kusini kwa mabao 4-1 katika michezo miwili ya nyumbani na ugenini huku Usm Algers ikiwatoa Asec Mimosas kwa jumla ya mabao 2-0 ikitoka suluhu ugenini na kushinda 2-0 nyumbani.
Katika mchezo huo wa fainali Yanga sc itaanzia nyumbani katika uwanja wa Benjamin Mkapa Mei 28 na marudiano yatafanyika nchini Algeria Juni 3 ambapo matokeo ya jumla ndio yatampoa mshindi kombe pamoja na medali za ubingwa ambazo zitakabidhiwa katika mchezo wa pili nchini Algeria.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Bingwa wa fainali hizo anatarajiwa kupata takribani shilingi bilioni 4.7 za kitanzania huku mshindi wa pili akipata shilingi bilioni 1.9.