Home Makala Yanga sc Waitungua Mbao Fc

Yanga sc Waitungua Mbao Fc

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Yanga sc imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mbao Fc katika mchezo wa kombe la shirikisho la Azam Sports uliofanyika katika uwanja wa Ccm Kirumba jijini Mwanza.

Katika mcheo huo uliotawaliwa na mvua kubwa Yanga sc iliwakosa mastaa kama Khalid Aucho,Heritier Makambo,Yanick Bangala,Djuma Shabani na Feisal Salumu kutokana na sababu mbalimbali ilitawala mchezo kwa asilimia 71 kipindi cha kwanza japo matokeo yalikua suluhu.

Kipindi cha pili Fiston Mayele alifunga bao dakika ya 53 akiunganisha krosi ya Farid Mussa alipokea pai fupi kutoka kwa Jesus Moloko na kumkuta Mayele aliyekua katikati ya mabeki wa Mbao Fc na kufunga kwa kichwa kikali.

banner

Yanga sc walitawala mchezo huo mpaka unaisha huku wakikosa mabao kadhaa ya wazi kupitia kwa Salum Abubakari,Fiston Mayele na Chico Ushindi na mpaka kipyenga cha mwisho matokeo yalibaki 1-0 na Mbao Fc kuyaaga mashindano hayo.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited