Home Makala Yanga sc Yaacha Msala Tanga

Yanga sc Yaacha Msala Tanga

by Sports Leo
0 comments

Kimenuka katika klabu ya Coastal Union ya Tanga baada ya kupoteza mchezo dhidi ya Yanga sc kwa mabao 2-0 katika mchezo wa ligi kuu nchini siku ya Jumapili iliyopita mchezo uliofanyika katika uwanja wa Mkwakwani uliopo katika ya mji.

Awali baadhi ya wadau wa michezo mkoani humo waliahidi kutoa zawadi ya kiasi cha Tsh 50. ambapo milioni 20 kati ya hizo zilitolewa na mkuu wa mkoa huo M.Adam Malima na zingine zikitolewa na matajiri wa mjini humo hasa wale wanaomiliki mabasi ya kusafirisha abiria.

Licha ahadi hizo Yanga sc ilifanikiwa kuondoka na ushindi na hivi sasa kumetokea mpasuko katika uongozi wa klabu hiyo ya Coastal union ambapo baadhi ya wanachama wa klabu hiyo wanahisi kuhujumiwa huku wakimtaja mwenyekiti wa klabu hiyo Steven Mguto kuwa ameshiriki kuwahujumu ili wapoteze mchezo huo.

banner

Kundi kubwa la wazee na wachezaji wa zamani wa klabu hiyo pamoja na wachezaji wa zamani wameungana pamoja kumshtumu Mwenyekiti Steven Mguto juu ya suala hilo huku wakipanga kufanya dua maalumu ya Albadili ili kumshtakia mungu

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited