Home Makala Yanga sc Yafuata Mrithi wa Mayele

Yanga sc Yafuata Mrithi wa Mayele

by Sports Leo
0 comments

Rais wa klabu ya Yanga sc Eng.Hersi Said amepanda ndege kimyakimya kwenda moja ya nchi za magharibi ya Afrika kwa ajili ya kusajili mshambuliaji atakayekuja kuziba nafasi ya Fiston Kalala Mayele ambaye anaondoka klabuni hapo.

Inasemekana safari hiyo ya kimyakimya ina lengo la kukamilisha dili la mchezaji Emmanuel Mahop raia wa Cameroon ambaye ni pendekezo la kocha mpya wa Yanga sc Miguel Gamond kama mrithi wa Mayele.

Emmanuel Mahop Dikongue ni mshambuliaji wa timu ya Canon Yaounde  ya nchini Cameroon ambapo msimu uliopita alimaliza akiwa amefunga magoli 11 na kutoa assisti nne katika ligi kuu ya soka nchini humo huku pia kwa msimu mzima akifunga mabao 28 katika michuano yote.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited