Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM Injinia Hersi Said ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindao Yanga, amesema wanaendelea na mchakato wa kusaka kocha mpya atakayerithi mikoba iliyoachwa na Cedric Kaze
Kumekuwa na tetesi kumuhusu kocha wa zamani wa Harambee Stars na Guinea ya Ikweta Sebastian Migne anayetajwa kumalizana na mabingwa hao wa kihistoria
Hersi amesema Migne ni miongoni mwa makocha wanaofanya nao mazungumzo lakini bado hawajafikia mwafaka
“Ni kweli, Migne ni miongoni mwa makocha ambao tuko katika mazungumzo nao, lakini hayuko peke yake, wengine wapo pia. Bado mwafaka haujafikiwa kuamua yupi tumkabidhi timu, “alisema Hersi
Awali Yanga ilikuwa na mpango wa kumuachia timu kocha Juma Mwambusi mpaka mwishoni mwa msimu
Hata hivyo wamebadili ‘gia angani’ wakiamua kumleta kocha mpya ambaye atafanya kazi na Mwambusi ili hata pale ligi itakapomalizika atakuwa amefahamu uimara na madhaifu ya timu yako wapi ili imsaidie katika kufanya maboresho