Kikosi cha klabu ya Yanga Sc kimeanza safari leo Mei 16 kuelekea Mkoani Tanga leo Asubuhi Mei 16 , 2025 na tayari kimewasili mchana huu kwa ajili ya mchezo wao wa nusu fainali ya Kombe la shirikisho la CRDB dhidi ya JKT Tanzania.
Mchezo huo wa nusu fainali Utakaopigwa Jumapili Mei 18, 2025 katika dimba la Mkwakwani mkoani Tanga majira ya saa kumi jioni.
Taarifa njema kwa Mashabiki wa klabu hiyo ni kurejea kwa Viungo wao Pacome Zouzoua na Khalid Aucho waliokuwa nje ya kikosi kutokana na Majeraha yaliyopelekea kukosekana kwenye mchezo uliopita wa NBC dhidi ya klab ya Namungo.