Klabu ya Yanga sc imefanikiwa kuibuka na ushindi mnono wa mabao 3-1 katika mchezo wa kirafiki wa kusherehekea siku maalumu ya klabu ya Rayon (Rayon’s day) uliofanyika katika uwanja wa Amahoro jijini Kigali nchini Rwanda na kuzua gumzo miongoni mwa mashabiki wa soka nchini humo.
Mchezo huo ilishuhudiwa kocha Roman Folz akianzisha mastaa wake wa kigeni akiwemo Andy Boyeli,Mousa Balla Conte,Mohamed Doumbia,Celestine Equa ambao walifanikiwa kuonyesha mchezo mzuri japo Yanga sc iliruhusu bao la mapema kutokana na makosa ya mlinzi Aziz Andabwile ambaye alirudisha kimakosa mpira uliokua wa kuanzisha mashambulizi na kujifunga mapema dakika ya pili ya mchezo kipindi cha kwanza.
Yanga sc ilisawazisha bao hilo kupitia kwa Boyeli aliyepokea pasi safi ya kupenyeza kutoka kwa Pacome Zouzoua dakika ya 28 na kuunyamazisha mashabiki wa Rayon Fc huku pia mshambuliaji huyo aligongeana pasi za haraka na Pacome na hatimaye kuandika bao la pili dakika ya 45 ya mchezo kwa shuti kali.
Kipindi cha pili kocha Roman Folz alifanya mabadiliko akiwaingia Offen Chikola na Lassine Kouma ambao waliongeza ubunifu katika kushambulia huku pia akimuingiza Prince Dube na kucheza na washambuliaji wawili uwanjani hali iliyowachanganya Rayon na kukubali bao la tatu la kichwa cha Bakari Nondo Mwamnyeto dakika ya 90+4.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Yanga sc licha ya kutawala mchezo huo pia ilikua na umiliki mzuri wa mpira japo haijacheza kwa kasi ile ambayo tumeizoea siku zote ambapo humshambulia mpinzani mara kwa mara.
Sasa tayari klabu hiyo ishaongeza kombe la kwanza msimu huu huku ikisubiri kuvaana na Simba Sc katika michuano ya Ngao ya Jamii nchini mwanzoni mwa mwezi septemba mwaka huu.