Home Makala Yanga sc Yaitwa Ikulu,Kupaa Mbeya

Yanga sc Yaitwa Ikulu,Kupaa Mbeya

by Sports Leo
0 comments

Kikosi cha klabu ya Yanga sc leo usiku kitakutana na Rais Samia Suluhu kwa ajili ya chakula cha jioni katika ikulu ya Magogoni jijini Dar es salaam baada ya kufanikiwa kupata medali ya michuano ya kombe la shirikisho nchini.

Yanga sc wamealikwa na Rais Samia kwa lengo la kuwapongeza kutokana na kuonyesha kiwango kizuri katika michuano hiyo ambapo wameingia fainali ya michuano hiyo baada ya miaka thelasini kupita tangu Simba sc walipofika katika hatua hiyo.

Yanga sc baada ya chakula cha jioni na Rais Samia kikosi hicho kitaelekea uwanja wa ndege kupaa kwenda Mbeya kwa ajili ya michezo miwili ya ligi kuu ya Nbc dhidi ya Mbeya City na Tanzania Prisons kisha watarejea Dar es salaam kwa ajili ya kwenda Tanga kwa ajili ya mchezo wa fainali wa kombe la shirikisho dhidi ya Azam Fc.

banner

Katika safari hiyo ya Mbeya,Yanga sc itatumia ndege maalumu ambayo imetolewa na Rais Samia ambapo mapema baada ya dhifa hiyo wataondoka usiku saa tano kamili.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited