Home Soka Yanga Sc Yajazwa Mamilioni

Yanga Sc Yajazwa Mamilioni

by Sports Leo
0 comments

Mastaa wa klabu ya Yanga sc wamefanikiwa kulamba Takribani Shilingi milioni mia tatu kutoka kwa mabosi wa klabu hiyo baada ya kushinda taji la kombe la Ngao ya jamii siku ya Jumapili.

Awali mastaa hao waliahidiwa kupata Shilingi milioni mia hamsini endapo wangeifunga Simba sc katika hatua ya nusu fainali na baada ya kuifunga 1-0 na kutinga fainali ambapo waliahidiwa kiasi kama hicho endapo wataifunga Azam Fc kitu ambacho kiliwapa hamasa na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 4-1.

Kutokana na matokeo hayo ambayo yaliwafurahisha mabosi wa klabu hiyo tayari mastaa hao wameingiziwa mamilioni hayo kwenye akaunti zao za beki na sass wameingia kambini siku ya leo kujiandaa na mchezo wa hatua za awali za michuano ya klabu bingwa barani Afrika dhidi ya Vital O ya Burundi siku ya Jumamosi katika uwanja wa Azam Complex Chamazi jijini Dar es Salaam.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited