Home Makala Yanga sc Yakomaa na Real Bamako

Yanga sc Yakomaa na Real Bamako

by Sports Leo
0 comments

Ilibaki kidogo tu Yanga sc ipate ushindi ugenini ilipokwenda kucheza na Real Bamako katika mchezo wa tatu wa kombe la shirikisho ambapo mchezo huo ulimalizika kwa sare ya 1-1 huku Yanga sc wakitawala mchezo huo kwa dakika zote tisini licha ya kuwa ugenini.

Yanga sc iliyoanza na kikosi kile kile kilichomfunga Tp Mazembe jijini Dar es salaam ilifanikiwa kupata bao dakika ya 60 likifungwa na Fiston Kalala Mayele akimalizia kazi nzuri ya Stephane Aziz Ki lakini bao hilo lilisawazishwa na Emil Kone dakika ya 90+1” kwa kichwa akiunganisha kona kutoka upande wa kushoto wa uwanja.

Yanga sc wangeshinda mchezo huo wangekua na uhakika wa kufuzu robo fainali moja kwa moja kwani wangefikisha alama sita huku tayari Tp Mazembe ameshapoteza alama tatu kwa kufungwa mabao 2-0 na Us Monastriene nyumbani mjini Lubumbashi.

banner

Msimamo wa Kundi hilo la D mpaka sasa Us Monastriene wapo kileleni kwa alama saba huku Yanga sc wakiwa nafasi ya pili na alama nne na Tp Mazembe wakiwa na alama tatu huku Real Bamako wakiwa wana alama mbili mkiani mwa msimamo.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited