Klabu ya Yanga sc imefanikiwa kufuzu hatua ya nusu fainali ya michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika ikiiondosha timu ya Rivers United ya nchini Nigeria kwa jumla ya mabao 2-0 katika michezo miwili ya nyumbani na ugenini.
Kuitoa Rivers United kwa idadi hiyo ya magoli mawili ni kulipa kisasi cha miaka miwili iliyopita ambapo pia Yanga sc iliondolewa kwa tofauti hiyo ya magoli mawili ikifungwa nyumbani na ugenini kwa bao 1-0 na kuondoshwa katika hatua ya pili ya michuano hiyo.
Yanga sc yenyewe ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa 2-0 ugenini nchini Nigeria mabao ya Fiston Mayele huku katika mchezo wa marudiano hapa nchini timu hizo zikitoka 0-0 licha ya Yanga sc kujitahidi kupata bao lakini juhudi hizo ziligonga mwamba mpaka dakika tisini zinatamatika uwanjani hapo.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Yanga sc sasa imeweka historia ya kufuzu hatua ya nusu fainali kwa miaka mingi ambapo katika mchezo huo itakutana na Malumo Gallant ya Afrika ya kusini ambayo imefanikiwa kuwatoa Pyramid Fc ya nchini Misri.