Klabu ya Yanga sc imemtambulisha rasmi mchezaji Offen Chikola ambaye amejiunga na klabu hiyo kwa mkataba wa miaka miwili akiwa kama mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake na klabu ya Tabora United.
Chikola amesaini klabuni hapo baada ya kuonyesha kiwango bora msimu ulioisha wa ligi kuu akifunga mabao saba pamoja na kuwa ni kiungo wa pembeni nafasi aliyocheza msimu mzima.
Mabosi wa Yanga sc wamekamilisha usajili huo ikitajwa kuwa anakwenda kuchukua nafasi ya Farid Mussa ama Dennis Nkane ambao wanaweza kuondolewa klabuni hapo kutokana na kukosa nafasi ya kucheza mara kwa mara.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Chikola anatarajiwa kuiongezea kasi safu ya ushambuliaji ya klabu hiyo akiungana na Clement Mzize na Prince Dube katika safu ya ushambuliaji ya klabu hiyo huku wakisaidiwa na Pacome Zouzoua atakayekua anacheza kama namba kumi akichukua nafasi ya Stephan Aziz Ki aliyeuzwa.