Klabu ya Yanga sc imemtambulisha beki Gift Fred ambaye imemsajili kama mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake na klabu ya S.C Villa ya nchini Uganda inayoshiriki ligi kuu nchini humo.
Yanga sc imemsajili beki huyo wa katikati ambaye anakuja kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Beki Mamadou Doumbia ambaye wapo kwenye mazungumzo ya kuvunja mkataba wake baada ya kiwango chake kutowaridhisha mabosi wakubwa pamoja na benchi la ufundi la klabu hiyo.
Doumbia licha ya kuwa alikua anapata nafasi katika timu ya Taifa ya wachezaji wa ndani wa Mali ameshindwa kupata namba mbele ya mabeki Dickson Job,Bakari Mwamnyeto na Ibrahim Hamad ambao walikua chaguo la kocha Nasredine Nabi.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Gift licha ya kuwa alikua ana uhakika wa namba katika kikosi cha Villa inampasa kupambana vya kutosha ili kupata nafasi katika kikosi cha Yanga sc ambacho kiko imara zaidi kulinganishwa na alikotoka.