Klabu ya Yanga sc imemtangaza rasmi mchezaji Nickson Kibabage kuwa mchezaji mpya wa klabu hiyo ikiwa ni usajili wake wa kwanza katika klabu hiyo kwa dirisha hili kubwa la usajili.
Yanga sc ambao ni mabingwa mara mbili mfululizo wa ligi kuu nchini wamepanga kuboresha kikosi chao katika maeneo machache ambapo mchezaji huyo atakua na manufaa katika maeneo ya beki wa kushoto na kiungo mshambuliaji kutokea pembeni ya uwanja.
Kibabage anatajwa kuigharimu Yanga sc zaidi ya Tsh.1oom ikiwa ni dau lake la usajili pamoja na gharama ya kuvunja mkataba wake na klabu ya Singida Fountain Gate Fc.
Mara baada ya kutambulishwa mchezaji huyo ameingia kambini ambapo mapema hivi leo ameungana na baadhi ya wachezaji wa timu hiyo kwenda nchini Malawi kwa ajili ya mchezo wa hisani kusherehekea sherehe za uhuru wa nchi hiyo ambapo Yanga sc imepata mwaliko maalumu.