Home Makala Yanga sc Yamtuliza Masau Bwire

Yanga sc Yamtuliza Masau Bwire

by Sports Leo
0 comments

Licha ya tambo za hapa na pale,jana msemaji wa Ruvu Shooting Masau Bwire alikua kimya baada ya mchezo wa Yanga sc dhidi ya timu yake kumalizika kwa Yanga sc kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Yanga sc inabidi wajilaumu wenyewe baada ya kukosa magoli kadhaa ya wazi hasa Penati ambayo ilipigwa na Deus Kaseke na kipa kufanikiwa kuipangua licha ya kuwa na bao la utangulizi lililofungwa na Michael Sarpong dakika ya 30 ya mchezo bao ambalo lilisawazishwa kutokana na makosa ya mlinzi Bakari Mwamnyeti yaliipatia Ruvu Shooting bao kupitia kwa David Richard dakika ya 59.

Kasi ya Tuisila Kisinda iliwasumbua mabeki wa Ruvu Shooting ambapo dakika ya 65 krosi yake ilisindikizwa na kichwa cha Cassian Ponera na kuipatia yanga ushindi katika mchezo huo wa raundi ya 14 na kuendelea kuongoza katika msimamo wa ligi nchini.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited