Home Makala Yanga sc Yamuwania Girumugisha

Yanga sc Yamuwania Girumugisha

by Sports Leo
0 comments

Taarifa kutoka Nchini Burundi zimethibitisha kuwepo na Mazungumzo baina ya klab ya Yanga sc na winga Raia wa Burundi anayeitumikia klabu ya Al Hilal Jean Claude Girumugisha (20) na mazungumzo hayo yanaripotiwa kuwa yamefikia pazuri.

Winga huyo hatari alikuwa kwenye rada za Wananchi tangu msimu uliopita na sasa wameonyesha kuwa siriazi na Usajili huo baada ya kuwavutia zaidi katika Michezo miwili ya klabu bingwa waliyocheza nao dhidi ya Al Hilal msimu hui,

Ndani ya Young Africans kuna baadhi ya wachezaji wakigeni wwataachana nao ikiwa ni pamoja na wale wanaomaliza mikataba nao ili kupata nafasi ya kumsajili winga huyo anayesifika kwasasa ndani ya klab Bingwa Afrika.

banner

Stephen Aziz Ki,Kennedy Musonda na Cletous Chama pamoja na Clement Mzize ni moja ya majina ambayo yanatarajiwa kuondoka klabuni hapo kutokana na kumaliza mkataba na wengine kuuzwa baada ya kuwepo kwa ofa nono.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited