Home Makala Yanga sc Yapanda Kimataifa

Yanga sc Yapanda Kimataifa

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Young Africans imepanda katika viwango vya (CAF) kutoka nafasi ya (75) hadi (46) huku pia klabu ya Simba SC imepanda kutoka nafasi ya (14) hadi nafasi ya (12).

Hayo yamekuja baada ya Yanga sc kufanikiwa kuifunga klabu ya Club Africains na kufuzu hatua ya makundi ya kombe la shirikisho baada ya kuibuka na ushindi wa 1-0 ugenini jijini Tunis huku Simba sc ikifuzu hatua ya makundi ya klabu bingwa barani Afrika baada ya kuitoa timu ya Premero Augosto ya nchini Angola kwa jumla ya mabao 4-1.

Yanga sc licha ya kutofuzu hatua ya makundi ya klabu bingwa Afrika kwa miaka 24 mfululizo hatimaye imeangukia katika kombe la shirikisho baada ya kutolewa na Al Hilal ya Sudan ambapo inatarajiwa kutoa ushindani wa maana katika kundi ambalo itapangwa hasa baada ya uongozi wa klabu hiyo kuwa na shauku ya kufanya vizuri zaidi.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited