Home Makala Yanga sc,Bruno Gomez Mambo Safi

Yanga sc,Bruno Gomez Mambo Safi

by Sports Leo
0 comments

Kilichobaki ni kumalizana kwa vilabu vya Yanga sc na Singida Big Stars ili staa Bruno Gomez atue jangwani msimu ujao baada ya kufikia makubaliano binafsi baina ya pande mbili za klabu ya Yanga sc na mchezaji huyo.

Picha kamili iko hivi,hivi karibuni staa huyo alitua jijini Dar es salaam na kufanya mazungumzo na mabosi wa Yanga sc ambapo alikubali kutua klabuni hapo huku wakielewana mpaka dau la usajili na kilichobaki sasa ni msimu umalizike ili klabu hiyo ifungue ukurasa wa mazungumzo na Singida Big Stars kuhusu bei ya staa huyo.

Inaaminika kwamba usajili huo ni pendekezo la kocha Nasredine Nabi aliyetaka mchezaji huyo kuja kuziba nafasi ya Feisal Salum ambaye nafasi ya kurudi kikosini humo imekua finyu.

banner

Mabosi wa Yanga sc wanaamini kwamba kumpata Bruno ni suala la muda tu kutokana na uhusiano mzuri na bosi mkubwa wa klabu hiyo ambaye ni mpenzi wa Yanga sc kindakindaki huku Afisa habari wa klabu hiyo Hussein Masanza akikanusha kuhusu uwepo wa dili hilo.

“Bruno ana mkataba wa miaka mitatu na timu inamhitaji sana, hatuna mpango wa kumuuza kwa sasa.” alisema Hussein.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited