Yanga Sc itakuwa na mchezo wa kirafiki kesho dhidi ya KMKM ya kisiwani Unguja,Zanzibar kwa ajili ya kujiandaa na raundi ya tano ya ligi kuu bara itakayochezwa Octoba ,3 uwanja wa Uhuru dhidi ya Coastal Union.
Mechi hiyo ya Kesho itachezwa katika kiwanja cha Azam Complex kilichopo Chamazi jijini Dar-es-salaam.
KMKM wamewasili leo jijini Dar-es-salaam na wamejiandaa vizuri kwaajili ya mchuano wa kesho dhidi ya Yanga,kwani nao wanajichua kwaajili ya ligi kuu Zanzibar inayotarajia kuanza hivi karibuni.