Timu ya Yanga sc imejichimbia kileleni mwa msimamo wa ligi kuu Tanzania bara baada ya kuifunga timu ya Jkt Tanzania kwa bao 1-0 katika mchezo wa ligi kuu Tanzania bara.
Deus Kaseke alifunga bao dakika ya 39 akipokea pasi nzuri ya mpenyezo kutoka kwa Yacouba Songne na kupeleka alama tatu kwa Yanga sc iliyoongeza alama tatu na kufikisha alama 31 katika uongozi wa ligi kuu nchini.
“Ninafurahi kucheza na Songne kwa kuwa nimejua aina ya uchezaji wake hivyo tunapambana kwa ajili ya timu na nimeshajua aina ya uchezaji wake,” Alisema Kaseke wakati akihojiwa na Vyombo vya Habari.