Home Makala Yanga Yapeleka Mashtaka Ya Morrison Tff

Yanga Yapeleka Mashtaka Ya Morrison Tff

by Sports Leo
0 comments

Uongozi wa klabu ya Yanga rasmi umepeleka malalamiko Shirikisho la soka nchini (TFF) kuhusu kushawishiwa winga wake Bernard Morrison kujiunga na klabu nyingine kinyume Cha sheria,ili haki itendeke na hatua stahiki ziweze kuchukuliwa.

Kaimu katibu Mkuu wa Yanga Wakili Simon Patrick amesema klabu haiwezi kufumbia macho maelezo yaliyotolewa na Winga huyo ambaye ameweka wazi kila kilichotokea. ‘….Mchezaji wetu ameeleza kila kitu,hivyo tumepeleka malalamiko yetu TFF na chombo husika kitasikiliza kutokana na ushahidi tuliouwasilisha na kutolea maamuzi.
Patrick amesema tayari ushahidi umekusanywa kwa ajili ya suala hilo ikiwa ni pamoja na kumhoji mchezaji na vielelezo vingine vinavyohusiana na suala hilo.

Source:Yanga App

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited