Home Makala Yanga Yashusha Mtaalamu Wa Viungo

Yanga Yashusha Mtaalamu Wa Viungo

by Sports Leo
0 comments

Wadhamini wa Yanga GSM wameendelea kulisuka benchi la ufundi baada ya kumshusha kocha wa viungo Riedoh Berdien ambaye pia atakuwa kocha msaidizi wa pili baada ya Boniface Mkwasa.

Berdien ametua nchini akiwa ni pendekezo la kocha mkuu Luc Eymael aliyewasili mapema wiki hii.

Raia huyo wa Afrika Kusini anatajwa kuwa mmoja wa wataalam bora kabisa kwenye eneo la kutunza utimamu wa kimwili wa wachezaji akiwa na uzoefu wa zaidi ya miaka 12, amefanya kazi katika mataifa sita tofauti barani Afrika.

banner

Karibuni alikuwa kocha wa viungo wa timu ya Taifa ya Wanawake ya Afrika Kusini maarufu kama Banyana banyana.

Wakati kocha Micho akitoka Orlando Pirates na kujiunga na Zamaleki alimpendekeza kuungana nae nchini Misri,Hata hivyo Berdien hakuwa tayari kufanya kazi nchini Misri.

Mafanikio yake ni kushiriki kombe la dunia la Wanawake akiwa na Banyana Banyana mwaka 2019 Pia mwaka 2018 alitwaa taji la Nedbank akiwa na Free State Stars iliyokuwa ikinolewa na Luc Eymael.

Mwaka 2017 akiwa na timu ya Taifa ya Togo, walifuzu fainali za AFCON 2017 Lakini pia ameshinda medali tatu za dhahabu kwenye michuano ya COSAFA akiwa na Banyana Banyana.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited