Home Makala Zahera Akubali Mziki Wa Mbeligiji Yanga

Zahera Akubali Mziki Wa Mbeligiji Yanga

by Dennis Msotwa
0 comments

Kocha wa zamani wa Yanga Mwinyi Zahera ameonyesha kukubaliana na mbinu za kocha mpya wa klabu ya Yanga Luc Aymael ambaye amejiunga na klabu hiyo hivi karibuni.

Kocha huyo Mbeligiji ni kocha aliyekuja kuchukua nafasi ya Zahera baada ya kuwa imekaimiwa na Bonifasi Mkwasa kwa miezi kadhaa tangu Zahera atimuliwe.

Akihojiwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini Zahera alikubaliana na mbinu za kocha huyo huku akisisitiza ni suala la muda tu ili wachezaji wazimudu.

banner

“Nimpongeze kocha kwa kuiwezesha Yanga kucheza mpira mzuri na wakuvutia tofauti na mchezo wao uliopita, naamini kama kocha atapewa nafasi ya kufanya kazi yake watakuwa na kikosi bora kwa misimu ijayo,” amesema Zahera

“Binafsi sikushangaa matokeo yao ya awali walipofungwa na Kagera Sugar, nilijua ni ugeni wa mbinu za kocha kwa wachezaji, lakini kwa sababu wachezaji wengi nawajua nilikuwa na matumaini ya kubadilika kwa kikosi katika mechi zinazokuja, kocha anastahili pongezi hizi”

Aidha Mcongomani huyo amesifu usajili wa kiungo mshambuliaji Bernard Morrison ambapo amesema mchezaji huyo atakuwa na mchango mkubwa kwenye kikosi cha mabingwa hao wa kihistoria

“Nimemuona mchezaji wao mpya waliomleta juzi (Morrison), ni mchezaji mzuri sana, Nadhani kama kocha ataweza kumtumia vizuri, atawasaidia”

“Mchezaji huyu akitumika vizuri pamoja na Molinga nadhani watafunga mabao mengi”Alisema Zahera ambaye yupo nchini kwa mapumziko.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited