Home Makala Zesco Wawasili,Lwandamina Agoma

Zesco Wawasili,Lwandamina Agoma

by Sports Leo
0 comments

Kikosi cha timu ya Zesco Fc kimewasili nchini usiku kikitokea nchini Zambia kuja kucheza na Yanga sc mchezo wa raundi ya kwanza hatua ya kwanza kuwania kufuzu hatua makundi ya klabu bingwa barani Afrika.

Mabingwa hao wa ligi kuu nchini Zambia walitua nchini Usiku wa kuamkia leo wakiwa na kikosi cha wachezaji 18 pamoja na viongozi wa benchi la ufundi na viongozi wa msafara.

Kocha George Lwandamina ambaye amewahi kuifundisha Yanga sc amesema hakupoteza muda kuangalia mikanda ya michezo ya Yanga sc kwa maana anatanguliza ubora wa kikosi chake japo msaidizi wake mmoja aliangalia mchezo baina ya timu hiyo na Ruvu shooting ambapo Yanga ilipoteza kwa 1-0.

banner

Yanga na Zesco zitakutana uwanja wa taifa jumamosi ya septemba 14 na mchezo wa marudiano utafanyika nchini Zambia baada ya wiki mbili.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited