Bondia Mtanzania Fadhili Majiha ‘Kiepe Nyani’ ambaye ni bingwa wa mkanda wa WBC Afrika ameweka rekodi ya kuwa Bondia wa kwanza nchini kupata hadhi ya nyota nne na nusu akivunja rekodi ya mabondia Hassan Mwanyiko na Tony Rashid katika Mtandao wa maalumu wa Takwimu za mabondia wa Boxrec.
Bondia huyo amefikia kiwango hicho wiki moja baada ya kushinda kwa pointi dhidi ya mpinzani wake Bongani Mahlangu wa Afrika Kusini katika pambano la Raundi 10 lililoffanyika katika ukumbu wa sabasaba wilayani Temeke.
Pamoja na kufikisha hadhi hiyo Pia ameingia kwenye orodha ya Mabondia 10 Bora Duniani uzani wa Bantam, akishika nafasi ya 7 kati ya 1,056.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Mwakinyo ndiye Bondia wa kwanza Nchini kufikia Hadhi ya Nyota 4 lakini kwa sasa ameshuka mpaka nyota 2 katika uzani wa Super Walter wakati Tony Rashid ana Nyota 2.5 katika Uzani wa Super Bantam.