Bondia kutoka nchini Ajentina Hugo Santillan mwenye umri wa miaka 23 amefariki dunia kutokana na majeraha aliyoyapata baada ya kupambana na Eduardo Abreau taarifa iliyothibitishwa na shirikisho la ngumi duniani.
Bondia huyo amefariki siku mbili baada ya bondia mwenye asili ya Urusi Maxim Dadashev kufariki kwa majeraha aliyopata baada ya kupambana na Subriel Matias katika pamboni lililiofanyika katika ukumbi wa Mgm nchini Marekani.
Bondia huyo alizirai katika ukumbi siku ya Jumamosi baada ya pigano lake la ukanda wa WBC dhidi ya Eduardo Javier Abreu nchini Argentina kuisha kwa sare.Alipelekwa hospitalini na kufanyiwa upasuaji lakini akafariki siku ya Alhamisi.