Bondia Mtanzania Hassan Mwakinyo amenyang’anywa mkanda wa ubingwa wa African Boxer Union (ABU) ambao alikua anaumiliki hivyo hana Mkanda wa Ubingwa licha ya kubaki Nafasi ya 14 ya Ubora Duniani Uzani wa Super Welter akiwa na nyota 4.
Bondia huyo amenyang’anywa mkanda huo ikiwa ni muda mchache tangu avuliwe na ule wa Ubingwa wa Mabara wa WBF miezi kadhaa iliyopita kutokana na sababu zile za kutopanda ulingoni kutetea mikanda hiyo kwa miezi sita kwa mujibu wa sheria za ngumi.
Katibu Mkuu wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBRC), Yahya Poli amesema mashirikisho yana Kanuni zake, kama bondia hatatetea mkanda kwa miezi 6 anavuliwa mkanda ili kuruhusu kupiganiwa na wengine.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Bondia huyo ambaye kwa sasa yupo kikazi nchini Marekani amesema kuwa kuvuliwa Ubingwa kwa kutopigana hakumuumizi, kwani kwake matokeo mabovu ingekuwa ni kuvuliwa ubingwa kwa kupigwa ulingoni.