Kamisheni ya ngumi za kulipwa nchini (TPBRC) imemfungulia bondia Hassan Mwakinyo kutoka kifungoni baada ya kufanyika kikao cha maridhiano baina ya kambi ya bondia huyo,Kamisheni na kampuni ya PAF Promotions ambayo ndiyo iliyopeleka malalamiko.
Hapo awali bondia huyo alifungiwa mwaka mmoja na kamisheni hiyo sambamba na kupigwa faini ya shilingi milioni moja za kitanzania huku pia kampuni ya PAF promotions ikimpeleka mahakamani bondia huyo kutokana na kuichafua baada ya kugomea pambano baina yake na Charles Indongo wa Namibia.
Maridhiano hayo yaliongozwa na Baraza la michezo la Taifa (BMT) ambapo bondia huyo alikiri makosa na kuomba radhi ndipo akafunguliwa.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Licha ya kusamehewa Bondia Mwakinyo ameandikiwa barua ya onyo kali endapo kama atarudia utovu wa nidhamu na kuvunja Katiba,Sheria,Kanuni na taratibu za ngumi za kulipwa hatutasita kumchukulia hatua kali za kinidhamu.