Mabondia Hassan Mwakinyo na Arnel Tinampay hii leo wamekamilisha zoezi la upimaji ambapo Mwakinyo amemzidi kilo 1 mpinzani wake Arnel Tinampay atakayepambana naye katika uzani wa Super Welter kesho kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Mwakinyo alikuwa na kilo 70.6 wakati Tinampay alikuwa na kilo 69.7, pia mabondia hao walipimaji wa afya zao chini ya madaktari kutoka hospital tatu za Temeke, Sanitas na Sali International.
Pambano hilo kali na la kusisimua nchini halitakua na kiingilio huku matarajio ya watanzania wengi ni kwa Mwakinyo kuibuka na ushindi.