Home Masumbwi Tyson Fury kustaafu tena Boxing

Tyson Fury kustaafu tena Boxing

by Sports Leo
0 comments

Bondia wa uzito wa juu duniani toka Uingereza Tyson Fury ametangaza kuwa atastaafu ngumi za kulipwa baada ya mapambano yake matano ya mwisho ndani ya miaka miwili.

Bingwa huyo anayeshikilia ubingwa wa WBC baada ya kumpiga Mmarekani Deontay Wilder mwaka 2020 ameeleza pia kuwa anatarajia kuingia kwenye ukufunzi wa mchezo huo wa ngumi mara baada ya kutundika gloves zake.

Fury ameyataja mapambano hayo ni mawili dhidi ya Muingereza mwenzake Anthony Joshua,pambano la tatu dhidi ya Deontay Wilder,lingine ni dhidi ya Dillian Whyte na la mwisho ni dhidi ya bondia mwenye maneno mengi Derek Chisora.Wilder amejipanga kubakia katika mchezo huo na kuwapa mafuzo mabondia chipukizi.

banner

Tyson alisema kuwa ”Nitakampomaliza kama bingwa labda baada ya mapambano matano hivi,nitapumzika,nitaingia kutengeneza vijana na tunaamini tutapata bingwa mpya wa dunia pengine bora zaidi kuliko mimi”.Kwangu ni maamuzi magumu sababu najua ni nini ambacho naweza bado kufanya nikiwa ulingoni”.Hivyo itakuwa ni changamoto haswa”.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited