Shirikisho la soka Afrika(CAF) limetangaza kuwa kwenye mashindano ya kombe la mataifa Afrika mwaka huu timu itakayokuwa na idadi ya wachezaji 11 kwa kikosi kizima itaruhusiwa kucheza hata kama haina kipa rasmi ndani ya wachezaji hao.
Hayo yamejiri baada ya baadhi ya mataifa yaliyokwenda kushiriki mashindano hayo kuripoti maambukizo ya Uviko-19 mapema kabla ya mechi kuanza na kutishia uhai wa mashindano hayo makubwa barani Afrika.
CAF wamesema kuwa ili kukabiliana na changamoto hiyo na kutokuharibu ratiba ya mashindano hayo,Taifa litakolokuwa na maambukizi mengi ndani ya kikosi lakini walio wazima wanafika 11 basi mechi itapigwa kama ilivyopangwa bila kuahirishwa isipokuwa pale tu idadi ya ambao hawajaambukizwa ikiwa chini ya 11.
Wachezajim kadhaa kama beki wa Senegal Kalidou Kolibaly na Ismair Sarr wamekutwa na maambukizi ya uviko-19 ndani ya kikosi hicho.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Michuano hiyo itaanza rasmi hii leo kwa mchezo wa ufunguzi kati ya wenyeji Cameroon dhidi ya Burkina Faso majira ya saa moja usiku saa za Afrika Mashariki.