Staa wa soka la Tanzania Ibrahim Ajib Migomba bado hajaeleweka wapi atakipiga msimu ujao baada ya kushindwa kufikia muafaka na matajiri wa kongo Tp Mazembe ambao iliaminika atajunga nao baada ya kutengewa dau nono.
Taarifa za awali zilidai kwamba kisa cha mchezaji huyo kutojiunga na wakongo hao ni kuwa na mkataba wa awali na Simba sc hivyo vipengele kumbana japo sasa imebainika ameanza mazungumzo na Yanga kuhusu kuongeza mkataba baada ya ule wa awali kuisha msimu huu.
Ajibu aliyefanya vizuri na timu hiyo kwa msimu huu akitoa pasi za mabao 16 na kufunga mabao 6 ya ligi kuu bara amefanya kikao na mabosi hao wa jangwani na kuwapa masharti ambayo wakitimiza tu anamwaga wino na imeripotiwa amefurahishwa baada ya kujua timu hiyo itashiriki michuano ya kimataifa mwakani.
Hivi karibuni makamu mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela alisema Ajib bado anahitajika klabuni na hata ripoti ya mkufunzi Mwinyi Zahera imeonyesha kuhitaji huduma yake.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Ajibu alijiunga na Yanga mwaka 2017 akitokea Simba Sc ambako alikua kisoka akitokea timu ya vijana ya timu hiyo.