Home Soka Ajibu Gonjwa,Kuikosa Kenya

Ajibu Gonjwa,Kuikosa Kenya

by Sports Leo
0 comments

Kiungo mshambuliaji wa Tanzania, Ibrahim Ajibu Migomba yuko hatarini kuukosa mchezo wa marudiano dhidi ya Kenya Jumapili mjini Nairobi kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) baada ya kuumia kwenye mechi ya kwanza.

Meneja wa Taifa Stars, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ amesema kwamba Ajibu yuko shakani kushiriki mchezo wa marudiano kutokana na maumivu ya goti.

“Tunaendelea vizuri na mazoezi, lakini bahati mbaya Ajibu naye ameingia kwenye orodha ya majeruhi, ameumia goti, hivyo hatuna uhakika wa kuwa naye kwenye mchezo wa marudiano,”alisema Cannavaro.

Ajibu anafanya idadi ya wachezaji majeruhi Taifa Stars kufika wanne, baada ya kipa Aishi Manula wa Simba SC, beki David Mwantika na kiungo Mudathir Yahya wote wa Azam FC ambao wote walikosa mechi ya kwanza.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited